WAKATI hapa nchini Waislamu
wakianzisha mkakati wa kuhakikisha vyakula na baadhi ya vipodozi vinaandaliwa
kwa kufuata miongozo ya imani ya Kiislamu kwa kuanzisha taasisi ijulikanayo
kama ‘Halal’, mfanyabiashara wa Uturuki ameanzisha duka la ngono, kupitia
mtandaoni, ambalo pia litafuata utaratibu wa ‘Halal’
Wasichana
wa Kiislamu waliovalia hijab wakipita mbele ya duka la kufundisha kujamiiana
lililoko katika mji wa Berlin, nchini Ujeruman, Julai 12, 2007
Pamoja na kuuza bidhaa nyingine,
duka hilo pia litatumika kutoa ushauri kwa Waislamu, wa jinsi ya ‘kujamiiana
kwa kufuata halal’, au kujamiiana kwa kufuata sheria za Kiislamu, yaani Sharia.
Mjasiriamali huyo Haluk Murat
Demirel, 38 ameanzisha kinachoitwa “Halal Sex Shop” baada ya rafiki zake
kumwambia kuwa wamekuwa wakihangaika kutafuta ushauri kuhusiana na kujamiiana
kwa kufuata utaratibu wa Kiislamu lakini hawapati.
“Mitandao mingi inaonesha tu picha
za ngono ambazo zinawachefua Waislamu. Mambo mengi ya maana katika eneo hilo la
kujamiiana hayapatikani. Yale ambayo yako kwenye mitandao hayajathibitishwa na
Waislamu,” Demirel aliwaambia waandishi wa habari.
Mtandao wa Demirel unaelezea
huduma unayoitoa ni salama na inaangukia katika sheria za Kiislamu. Ukiingia
katika mtandao huo, watumiaji wanashauriwa kuchagua kubonyeza kidude kimoja
kama ni wanawake, au ubonyeza kidude kingine kama ni wanaume, na wanaelekezwa
kufuata kurasa kutegemea na jinsi zao. Vichwa vya habari katika tovuti hiyo ni
pamoja na “Kujamiiana katika Uislamu”, “Maisha ya kujamiiana katika Uislamu”,
na “Mapenzi ya kunyonyana kulingana na Uislamu.”
Huduma au bidhaa katika tovuti hiyo
zinapatikana kwa malipo ya dola za Marekani, fedha za Uturuki (liras) au euro,
na kila bidhaa inayonunuliwa kupitia tovuti hiyo huambatanishwa na kijitabu
kidogo chenye maelezo kuhusu kujamiiana kwa kufuata Uislamu.
Waanzilishi wa tovuti hiyo
wameandika katika tovuti hiyo kuwa, ingawa watu wengi wanadhani Uislamu
uko kinyume na mambo ya kujamiiana, ukweli ni kwamba dini hiyo
“inakubaliana na kujamiiana katika mazingira yaliyokubalika, kakma vile kwa
wanandoa.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari,
yapo maduka machache sana ‘yanayouza huduma kama hiyo’ nchini Uturuki, nchi ya
Kiislamu lakini yenye katiba inayofuata mfumo wa kisekula.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Tayyip
Erdogan mara kwa mara amekuwa akikosolewa kwa kuachia hali hiyo; yeye amekuwa
akipendekeza kuwa maduka hayo yaitwe ‘ maduka ya mapenzi’, pia amewashauri
wanawake wawe wanazaa idadi maalum ya watoto, huku akizuia vikali utoaji mimba
nchini humo.
Hapa nchini, wakati mvutano wa nani
mwenye haki ya kuchinja ulipokuwa ukizidi kupamba moto, Waislamu walikuwa
wakikamilisha kazi ya kusajili chombo kitakachokuwa na wajibu wa kuhakikisha
kuwa vyakula na vipodozi vinaandaliwa kwa kufuata ‘Halal’.
Baadhi ya makampuni ya juisi na
vyakula mbalimbali yameanza kufungisha bidhaa hizo kwa kutumia vifungashio
vyenye nembo ya ‘Halal’ ili kuthibitisha kuwa vinafaa kutliwa au kutumiwa na
Waislamu.
0 comments:
Post a Comment