Na Mwandishi Wetu
KANISA la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), limeandaa maombi maalum ya siku mbili yenye lengo la kuwaombea baraka watu katika kipindi cha mwaka 2014, ambayo yatafanyika tarehe 11 na 12 mwezi huu katika makao makuu ya kanisa hilo Mwenge, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa vipeperushi vinavyotangaza kuwepo kwa maombi hayo yatakayoongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Zachary Kakobe, watu watakaohudhuria maombezi hayo wanatakiwa kuvaa mavazi ya heshima ili kudhihirisha kuwa wanamheshimu Mungu wanayekwenda kumwomba.
“Watakaovaa milegezo, vimini, jeans, nywele bandia hawataruhusiwa kuingia kanisani. Wanawake wafunike vichwa vyao na wanaume wasivae kofia nyumbani mwa BWANA. (1 Wakorintho 11:4-5,10) linasema tangazo linalowaalika watu katika maombi hayo.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, maombi yatakuwa yanaanza saa 9:30 adhuhuri hadi saa 12:30 jioni. Limeeleza kuwa, kila atakayehudhuria maombi hayo aende na mahitaji yake 10 ambayo Askofu Kakobe atayaombea kwa jina la Yesu.Inaelezwa kuwa, maombi ya namna hiyo huwa ni ya kipekee na kuna shuhuda nyingi ya matendo ya Mungu kupitia maombi hayo.
Home
»
»Unlabelled
» KARIBU KWENYE MAOMBI YA MIUJIZA, USIVAE MLEGEZO WALA JEANS!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment