Na Mwandishi Wetu
MCHUNGAJI mmoja ambaye alijaribu kumuiga Yesu Kristo katika muujiza wa kutembea juu ya maji, amezama majini katika pwani ya magharibi ya Afrika, hivi karibuni.
Mchungaji Frank Kabele, 35,ameripotiwa kuwa aliwaambia waumini katika kanisa analoliongoza kuwa, atafanya muujiza huo na baadaye kwenda katika ufukwe wa bahari katika mji mkuu wa Gabon, Libreville.
Kabele aliliambia kusanyiko lake kuwa, alikuwa na ufunuo na ana imani kuwa ataweza kutembea juu ya maji kama Yesu alivyofanya. (Mathayo 14:22-33), mmoja wa waumini aliwaambia waandishi wa habari.
Alisema kuwa, siku ya tukio Mchungaji Kabele aliwachukua waumini hadi baharini akasema angeweza kutembea juu ya maji kuanzia mahali walipokuwa wamesimama hadi eneo linalojulikana kama Komo, umbali ambao boti huchukua dakika 20 kufika.
“Aliingia katika maji ambayo baadaye kidogo yalimzidi na hakuweza kuonekana tena,” alisema mtoa habari huyo.
Home
»
»Unlabelled
» MCHUNGAJI AFIA BAHARINI AKIMWIGA YESU KUTEMBEA JUU YA MAJI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment