Na Agness Mayagila, Arusha
Maelfu ya wanawake na mabinti kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,
na maeneo jirani wamemiminika katika uwanja wa sheikh Amri Abeid mjini Arusha
ili kujumuika kwa pamoja kumkataa jini mahaba ambaye wamedai amewatesa wanawake
wengi na hivyo kuleta shida katika ndoa zao.
Aidha wanawake wengi walimiminika na kujaza uwanja huo mpaka
nje kuonesha namna ambavyo wamechoka na mateso ya mwovu shetani ambapo
walipata fursa ya kumwabudu Mungu na kuingia katika maombi ya mzigo ili
kumpinga jini anayewatesa
Akifundisha katika kusanyiko hilo la aina yake Jumamosi
iliyopita, Mtumishi wa Mungu Jovin Msuya alisema kuwa, maneno
mengi,kelele na kutotimiza wajibu kwa wanawake ni chanzo kikubwa cha
wanawake wengi kuteswa na jini mahaba jambo ambalo limeleta uharibifu mkubwa
katika ndoa za walio wengi na wengine kushindwa kuhimili na kuacha ndoa zao.
Jovin ambaye ni Meneja wa kituo cha redio ya Kikristo cha Safina
FM kilichoandaa kusanyiko hilo, alisema kwamba wanawake wengi hawatimizi wajibu
wao kwa waume zao na hivyo kutoa mianya ya adui kupenyeza tabia zake katikati
yao na hivyo kusababisha faraka na magomvi katika ndoa zao
Alisema kwamba wakati umefika kwa wanawake kuamua kwa dhati
kutimiza wajibu wao ndani ya ndoa zao ili kuziba nafasi ambazo adui
anaweza kuzitumia kuzipiga ndoa zao ambapo alibainisha kwamba wanawake
wengi hawafanyi wajibuwao ipasavyo na ndio mwanya wa adui shetani
Akinukuu katika maandiko matakatifu kutoka Mithali 7:
Mtumishi Jovin alisema kwamba jini mahaba anapomwingia mtu
ni lazima aisome tabia ya wanandoa na kujua yale wanayoyapenda ili
awafanyewasiyafanye na kujifanya mshirika (mwili mmoja) kwa kusudi la kuwapata
wanandoa kwa urahisi
Katika hatua nyingine aliwataka wanawake kufanya bidii kumwomba
mungu ili kurejesha mioyo ya waume zao kwao ikiwa ni pamoja na kuziba mianya ya
adui katika ndoa zao
'Wanawake ni lazima mzibe nafasi ambazo adui anazitumia
kuwaingia,timizeni wajibu wenu kwa waume zenu,mnasema uchawi unatumika
kuwakamata waume zenu someni neno mjua kuishi na waume zenu'alisema jovin
Aliongeza kwamba wanaume hawapendi maneno mengi na kelele za
wanawake ambazo alizitaja kuwa zinawafanya wanaume wengi kuchelewa kurudi
majumbani na kuwaasa wanawake kujichunguza upya na kumwomba Mungu awasaidie
Alisema hakuna uchawi wa kumkamata mwanaue bali ni kutimiza yote
ayatakayo,kwa wao kuwa wasafi waowenyewe,mazingira,mapishi bora na engine
yaliyo wajibu wao na kwamba wataona mabadiriko kwa waume zao
Aidha, kongamano hilo liliongozwa na kichwa kisemacho “Ukweli
kuhusu vita ya mwanamke” ambapo lilipambwa na waimbaji mbalimbali wa kike
wa nyimbo za injili.
0 comments:
Post a Comment